Serikali yawaajiri walimu 76,765 zaidi ili kufanikisha mfumo wa CBC

  • | KBC Video
    36 views

    Walimu 76,765 wameajiriwa na kupelekwa kwa Shule za msingi ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu na kuwaelekeza wanafunzi katika uchaguzi wa taaluma zifaazo. Tume ya walimu humu nchini inatoa wito wa mafunzo ya kitaaluma kwa walimu wanaotatizika katika kufundisha baadhi ya masomo ya mfumo huo. Akizungumza wakati wa mdahalo wa kaunti kuhusu mageuzi sekta ya elimu ambapo mwongozo wa mpito wa wanafunzi wa gredi ya 9 hadi shule ya upili ulizinduliwa, waziri wa Elimu Julius Ogamba alisisitiza haja ya ushirikiano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi wanapochagua taaluma watakazosomea.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive