Shabiki wa Timu ya DRC Leopard aeleza furaha yake kwa ushindi dhidi ya Taifa Stars

  • | VOA Swahili
    935 views
    Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa marejeano wa kufuzu fainali za AFCON 2025 dhidi ya DR Congo kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.⁣ Mabao ya Congo yamefungwa na mshambuliaji Meshack Elia katika dakika za 88 na 90+, nyota huyo akiitumikia Young Boys ya Uswisi katika ngazi ya klabu.⁣ Licha ya kupoteza mashabiki wa Stars wamezungumzia mchezo huo wakiipongeza timu hiyo.⁣ Hadi sasa kwenye msimamo wa kundi H, linaongozwa na DR Congo wenye pointi 12 ambao tayari wamefuzu kwenye fainali hizo, Tanzania (Taifa Stars) nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, Guinea nafasi ya tatu pointi 3, Ethiopia ikishika mkia ikiwa na pointi 1. Shabiki wa timu ya DRC Leopard alikuwa na haya ya kusema baada ya ushindi... ⁣ ⁣ #tanzania #afcon2025 #drc #naibuwaziri #hamismwinjuma #daressalaam #benjaminmkapa #uwanja #mashabiki #uingereza