Shaka la Shakahola

  • | Citizen TV
    2,231 views

    Ni mwaka wa pili sasa tangu mauaji mabaya zaidi ya itikadi za kidini nchini kushuhudiwa katika msitu wa Shakahola, na kusababisha vifo vya takriban watu mia tano. Familia ambazo zimekuwa zikisubiri kuwazika jamaa zao zikisalia bila mwelekeo, huku maiti zikisalia kwenye hifadhi ya maiti ya Malindi. Kwa familia hizi, serikali haijaonekana kukamilisha zoezi la kuwatambua jamaa zao hadi sasa. Francis Mtalaki amezungumza na familia ambazo ziliwapoteza jamaa kuzungumzia masaibu, mashaka na hata shaka ya mwisho wa zoezi hili kwenye makala haya ya SHAKA YA SHAKAHOLA