Shambulizi la angani la Israel lapiga shule ya UN

  • | VOA Swahili
    245 views
    Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya angani Alhamisi katika shule ya Umoja wa Mataifa katikati ya Gaza ambapo maafisa wa afya wa Palestina walisema watu wasiopungua 27 waliuwawa. Majeshi ya Ulinzi ya Israel yalisema wapiganaji wa Hamas walioshiriki katika shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel walikuwa wanaitumia shule hiyo kama maficho yao na “kuendesha vitendo vya ugaidi” kutoka eneo hilo. Ofisi ya habari ya Hamas ilitupilia mbali taarifa ya Israel na kusema kuwa majeshi ya Israeli yalifanya “uhalifu wa kinyama” dhidi ya watu waliokuwa wamekoseshwa makazi. Shambulizi hilo lilitokea katika shule inayoendeshwa na shirika la UN linalowashughulikia wakimbizi wa Palestina huko katika mji wa Nuseirat. Jeshi la Israel Jumatano lilitangaza kuanza “shughuli za operesheni zinazolenga” eneo karibu na sehemu hiyo hiyo, ikiwa baadhi ya maeneo ya Deir al-Balah na kambi ya wakimbizi ya Bureij. Jeshi hilo lilisema ilikuwa inashambulia malengo ya kigaidi, ikiwemo maeneo ya kijeshi, maghafala ya kuhifadhi silaha na miundombinu ya chini ya ardhi.” Wakazi wa eneo hilo waliripoti mashambulizi mazito ya mabomu. Watu wasiopungua 70 walikufa na wengine 300 walijeruhiwa kuanzia Jumanne, kufuatia “mashambulizi mazito yaliyofanywa na Israel” katikati ya Gaza, kulingana na jumuiya ya Madaktari Wasiokuwa na Mipaka. Watu kumi na moja walijeruhiwa Jumatano baada ya mji ulioko kaskazini mwa Israel uliposhambulia kutoka Lebanon, huduma za matibabu ya awali za Magen David Adom ya Israel zilisema. Kikundi cha wanamgambo wa Lebanon Hezbollah kilisema kililenga kundi la maafisa wa kijeshi kwa kutumia droni kujibu shambulizi lililofanywa na Israel. Mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Hezbollah yalianza Octoba 8. Tangu wakati huo, watu kiasi cha 400 wameuawa nchini Lebanon, wengi wao wapiganaji, na 25 upande wa Israel. Hamas ilianzisha shambulizi la kigaidi Oktoba 7 ndani ya Israel, ikiwauwa watu takriban 1,200, kulingana na majumuisho ya hisabu iliyotolewa na Israel, na kuwachukua mateka kiasi cha watu 250. Takriban mateka 120 wamesalia ndani ya Gaza, huku jeshi la Israel likisema 37 kati yao wamefariki.   Mashambulizi ya mabomu ya kulipiza kisasi yanayofanywa na Israel na mashambulizi ya ardhini yameuwa watu wasiopungua 36,500 huko Gaza, wengi wao raia, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza.   Baadhi ya taarifa katika repoti hii imetokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters. #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #unrwa #un