SHAMBULIZI LA ISRAEL LAUUA WATU 16 GAZA

  • | VOA Swahili
    403 views
    Maafisa nchini Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Isreal yameuua watu 16 katikati mwa Ukanda wa Gaza, wakiwemo wanawake watano na watoto wanne. Shambulizi la mapema leo Jumatatu asubuhi limeharibu nyumba katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat iliyojengwa katikati mwa Gaza na kuua takriban watu 10 wakiwemo wanawake wanne na watoto wawili. Katika Hospitali ya Awda ambayo ilipokea miili, imethibitisha idadi hiyo na kusema kuwa watu wengine 13 walijeruhiwa. Taarifa za hospitali zinaonyesha kuwa watu waliokufa ni pamoja na mama mmoja , mtoto na ndugu zake wengine watano. Shambulizi jingine katika nyumba kwenye mji wa Gaza limeuua watu sita akiwemo mwanamke na watoto wawili kwa mujibu wa kikosi cha ulinzi wa raia na wafanyakazi wa afya wanaofanya kazi chini ya serikali ya Hamas inayoongoza. Shambulizi la hivi punde katika mzozo wa miongo kadhaa kati ya Israel na Hamas ulichochewa Oktoba 7 wakati kundi la Palestina la Hamas liliposhambulia Israel, na kuua watu 1,200 na kuchukua mateka wapatao 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israel.⁣ Mashambulio yaliyofuata ya Israel dhidi ya eneo linalotawaliwa na Hamas tangu wakati huo yameua zaidi ya Wapalestina 40,000, kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo hilo, huku pia ikiwafukuza karibu watu wote milioni 2.3, na kusababisha baa la njaa na kusababisha madai ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Dunia ambayo Israel inakanusha. - AP, Reuters⁣ #gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina ⁣⁣