Sherehe za Eid-al Fitr: Waislamu wakamilisha mfungo wa mwezi wa Ramadhan

  • | Citizen TV
    959 views

    Waislamu nchini wameungana na wenzao ulimwenguni kote kusherehekea Eid ul-Fitr, tukio linaloashiria mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Kwa kushiriki sala za kipekee katika maeneo mbalimbali ya nchi, viongozi wa kidini na kisiasa wa Kiislamu walitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa amani, mshikamano, na maridhiano. Katika hotuba zao, walitoa wito wa kuwa na mshikamano wa kitaifa huku wakihimiza huruma na undugu kati ya wananchi wote