Shughuli ya bunge ya kukusanya maoni kuhusu hoja ya kumng'atia naibu rais Gachagua yakamilika

  • | K24 Video
    128 views

    Shughuli ya bunge ya kukusanya maoni kuhusu hoja ya kumng'atia naibu rais Rigathi Gachagua imekamilika leo huku idadi ya wakenya inayomtaka rais William Ruto aondolewa ofisini pamoja na naibu wake ikiongezeka. Wakenya hao waliozungumza katika vikao vya umma vilivyofanyika katika maeneo mbali mbali nchini wamesema kuwa utakuwa ni ubinafsi mkubwa endapo Gachagua atabanduliwa ofisini peke yake bila ya rais aliyechaguliwa naye.