Shule zilizotia fora zamani katika eneo la Nyatike zaandikisha matokeo duni

  • | Citizen TV
    119 views

    tukigeukia masuala ya elimu ni kuwa, baadhi ya shule ambazo zilikuwa mabingwa wa elimu katika kaunti ndogo ya Nyatike, Kaunti ya Migori sasa zinalaumiwa Kwa kuwasilisha matokeo Duni.. Shule ya upili ya Agenga, shule ya wavulana wa Moi Nyatike na shule ya upili ya Kibuon ni miongoni mwa shule zilizokuwa zinang'aa hapo awali kwenye mitihani ya KCSE. Shule ya upili ya Agenga ilikuwa na wanafunzi 7 pekee waliopata alama ya wastani ya C kwenda juu katika mtihani wa KCSE wa 2024 huku Moi Nyatike na Kibuon zikikosa hata mwanafunzi mmoja aliyepata alama ya wastani ya C.