Siku ya uhandisi duniani : Wahandisi wa kike wawanasihi wanafunzi

  • | KBC Video
    7 views

    Ulimwengu unaposherehekea siku ya uhandisi duniani, wanawake wahandisi humu nchini wamechukua hatua ya kuwanasihi wanafunzi wa shule za sekondari msingi kwa kuwapa maarifa kuhusu taaluma ya uhandisi. Akiongea wakati wa mpango wa unasihi katika shule ya msingi ya Utumishi Sacco eneo la Kitengela, afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya wahandisi, mhandisi Moreen Auka alikariri umuhimu wa mpango huo akisema unanuiwa kuwamotisha wasichana kusomea kozi za kisayansi na pia kuwa katika nafasi nzuri ya kuchagua taaluma. Mpango huo wa unasihi unaotekelezwa na wanawake wahandisi unadhamiriwa kuziba pengo lililopo katika sekta ya uhandisi ambapo idadi ya wanawake ni ndogo mno.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive