A Silent War: Ni hadithi za Mateso na Ustahamilivu wa Watu Nchini Congo

  • | VOA Swahili
    607 views
    A Silent War: Ni hadithi za Mateso na Ustahamilivu wa watu nchini Congo” ni makala yenye kukupa shauku kujua zaidi ikiangazia mgogoro wa kibinadamu unaoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) hasa eneo la mashariki mwa nchi. Katika maelezo ya dakika 28 yenye hisia nzito, makala hii inaangalia kwa undani maisha ya watu ambao wamekoseshwa makazi kutokana na mashambulizi ya muda mrefu ya wanamgambo na operesheni za kijeshi, ikibainisha uzito wa athari ya mgogoro huu kwa Wacongo. Makala hii ilitengenezwa katika mji wa Goma, ambapo watu wengi wamelazimika kukimbia makazi yao na shughuli za kipato chao. Ikikuletea ushahidi wa moja kwa moja kutoka kwa watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi yao (IDPs), inatoa taswira kamili ya watu walivyokuwa wanaishi hapo awali kwa amani katika makazi ya miji yao. Makala hii inakupitisha katika hatua mbalimbali za mgogoro huu, zikiwepo shutumu dhidi ya taasisi na watu mbalimbali, ikiwemo serikali ya Congo, Jeshi la Rwanda, na makundi yenye silaha ya waasi kama vile M23. #voa #voaswahili #vita #drc #mauaji