Siri ya maisha ya mrembo wa Instagrama aliyefungwa jela

  • | BBC Swahili
    938 views
    Mwanamitindo wa zamani wa Brazil na mshauri wa maisha ya kiroho Kat Torres amehukumiwa kifungo cha miaka nane jela Brazil baada ya kukutwa na hatia ya biashara haramu ya kusafirisha binadamu na kuwafanyisha kazi za utumwa. Kat Torres alikuwa na zaidi ya wafuasi milioni moja kwenye Instagram wakifuatalia maisha yake kutoka katika umaskini uliokithiri akiwa Brazil, hadi kuwa mwanamitindo wa kimataifa barani Ulaya na maisha ya anasa nchini Marekani. Lakini nyuma ya machapisho hayo mitandaoni kuna nguvu za giza, unyanyasaji wa kingono na biashara ya binadamu. #bbcswahili #bbceye #brazil Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw