Kwa nini watu wameisahau Sudan, miaka miwili tangu vita kuzuka?

  • | BBC Swahili
    352 views
    Leo imetimia miaka miwili tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza nchini Sudan. Umoja wa Mataifa unasema miili ya wanawake imekuwa kama uwanja wa vita nchini humo kwani ubakaji unatumiwa mara kwa mara kama silaha ya vita. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema uhalifu unatekelezwa na jeshi la Sudan pamoja na wapinzani wao, ambao ni wanamgambo wa Rapid Support Forces, RSF.