Tanzania kuendelea kuchimba, kuuza makaa ya mawe.

  • | BBC Swahili
    6,384 views
    Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuchimba na kufanya biashara ya makaa ya mawe kutokana faida za kiuchumi kwa taifa hilo, licha ya bidhaa hiyo kuhusishwa na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Baadhi ya mataifa barani Ulaya yanaachana na matumizi ya makaa ya mawe hususani katika kuzalisha umeme. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati, Doto Biteko katika mahojiano maalumu na mwandishi wa BBC Florian Kaijage, ambapo miongoni mwa mambo mengine aliyoyazungumzia ni pamoja usambazaji wa gesi majumbani, bei ya mafuta ya petroli na dizeli, kuwepo kwa umeme wa kutosha na masuala ya uongozi kwa ujumla. #bbcswahili #nishati #gesi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw