Trump asema atainunua Gaza

  • | BBC Swahili
    1,068 views
    Kundi la Hamas limesema kwamba limesimamisha shughuli ya kuwaachilia mateka kutoka Gaza siku ya Jumamosi kama ilivyotarajiwa. Hamas inasema hali hii itakuwa kwa muda usiojulikana kwa sababu inadai kwamba Israel imekiuka makubaliano ya kusitisha vita kwa kuchelewesha mpango wa Wapelestina kurudi nyumbani kaskazini mwa Gaza. Israel nayo imejibu kwa kusema tangazo hilo linakiuka makubaliano ya amani ya Gaza. Wakati hayo yakijiri, Rais wa Marekani Donald Trump amesema atachukua udhibiti wa Gaza na kuwaondoa Wapalestina kutoka eneo hilo - akisema amejitolea "kununua na kumiliki Gaza".