Tuju ataka majaji wa mahakama ya juu wachunguzwe

  • | KBC Video
    44 views

    Aliyekuwa waziri Raphael Tuju anataka tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini kuwachunguza majaji 5 wa mahakama ya upeo kwa madai ya upendeleo katika kesi inayohusisha mzozo wa mali. Tuju amesema naibu jaji mkuu Philomena Mwilu na majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u na William Ouko walikuwa wamefanya uamuzi wao tayari walipojiondoa kutoka kesi hiyo na kudumisha uamuzi wa mahakama ya rufani uliodhinisha kunadiwa kwa hoteli yake kwa kushindwa kulipa deni la shilingi bilioni 4.5 alilodaiwa na Benki ya ustawi wa Afrika ya Mashariki. Hata hivyo, afisa mkuu mtendaji wa EACC Abdi Mohamud amesema tume hiyo bado haijapokea ombi la Tuju.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive