'Tunaishi kwa kazi hii ya kuimba na watoto tunasomesha'

  • | BBC Swahili
    213 views
    Ulemavu umewanyima wengi fursa ya kuonesha ukubwa na ubora wa karama walizo jaaliwa, lakini kwa Daniel Maige na kundi lake ulemavu sio kikwazo, kwani licha ya kutoona wanatumia vipawa vyao vya muziki kutunga nyimbo na kupiga ala mbalimbali za muziki kwenye Barabara za Jiji la Dar es salaam. Kwa Mara ya kwanza Daniel na wenzake walingia barabarani mwaka 2015 na tangu wakati huo hadi hii leo wanaendelea kuudhiirishia ulimwengu kuwa wamejaliwa karama za kipekee licha kukabiliana na changamoto mbalimbali kama vile usafiri, uchakavu wa vifaaa na hata kadhia ya kufurushwa na askari wa jiji baadhi ya maeneo. Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds aliwatembelea na kuandaa tarifa ifuatayo. #bbcswahili #tanzania #ulemavu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw