"Tutakopa zaidi" Rais William Ruto asema

  • | NTV Video
    2,857 views

    Rais William Ruto alisema nchi italazimika kukopa zaidi ili kuendelea kuendesha serikali kufuatia kukataliwa kwa mswada wa fedha wa mwaka wa 2024 uliokusudiwa kupata pesa zaidi kupitia ushuru. Wakati wa mahojiano na wanahabari hapo jana, Ruto alisema serikali italazimika kukopa zaidi ya shilingi bilioni 346 ili kujaza nakisi hiyo, na hivyo kufanya jumla ya mikopo ya mwaka wa fedha wa 2024/25 kufikia karibu shilingi trilioni moja. Hii hata hivyo inakinzana na agizo lake kwa hazina ya kupunguza matumizi kwa kiasi sawa maswali yakiibuka kuhusiana na ahadi ya Rai Ruto kubana matumizi katika serikali yake .

    Subscribe to NTV Kenya channel for latest Kenyan news today and everyday. Get the Kenya news updates, discussions and other exciting shows.

    Website: ntv.nation.co.ke || Paper: Daily Nation || Twitter: @ntvkenya || Facebook: NTV Kenya || Instagram: NTV Kenya