- 631 viewsRais wa Kenya William Ruto Ijumaa alimteua waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kuwa naibu wake mpya, siku moja baada ya baraza la Seneti kupiga kura ya kumtimua naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua. “Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais, kuhusu kuteuliwa kwa Profesa Kithure Kindiki kushika nafasi hiyo ambayo imetokea afisini,” Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula alisema Ijumaa, akiwahutubia wabunge mjini Nairobi. Gachagua, ambaye alikanusha mashtaka yote dhidi yake wakati wa kesi ya kuondolewa madarakani, alimuunga mkono Ruto katika ushindi wake wa 2022 na kusaidia kupatikana kwa kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la kati mwa Kenya. Lakini katika miezi ya hivi karibuni , Gachagua amezungumza kuhusu kutengwa, huku kukiwa na taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari kuwa ametofautiana na Ruto wakati miungano ya kisiasa ikibadilika. Kindiki, mshirika wa karibu wa Ruto, ameshikilia wadhifa wa wizara ya mambo ya ndani katika kipindi chote cha miaka miwili ya Ruto kama rais. Hapo awali aliwahi kuwa seneta wa Kaunti ya Tharaka Nithi na alikuwa mgombeaji mkuu kuwa mgombea mwenza wa Ruto wakati wa uchaguzi wa 2022. Baadaye Bunge litalazimika kupiga kura kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kabla ya kuapishwa. #Kenya #seneti #gachagua #kindiki #voa #voaswahili
'...Uamuzi uliochukuliwa haukuwa na ukabila...'
- - Duniani Leo ››
- 21 Apr 2025 - The death of Pope Francis on Monday sets in motion centuries-old traditions which will culminate in the election by cardinals of a new pontiff -- but with a few changes.
- 21 Apr 2025 - Here are some key dates in the life of Pope Francis, the first Jesuit and Latin American pope, who died on Monday aged 88:
- 21 Apr 2025 - Pope Francis, the first Latin American leader of the Roman Catholic Church, has died, the Vatican said in a video statement on Monday.
- 21 Apr 2025 - The 88-year-old pontiff died at his home at his residence in the Vatican's Casa Santa Marta.
- 21 Apr 2025 - Embakasi East Member of Parliament (MP) Babu Owino has suggested a potential joint presidential bid in 2027 with his Kiharu counterpart Ndindi Nyoro.
- 21 Apr 2025 - Key quotes from Pope Francis’s papacy: – Humility – “Pray for me” – pronounced at the end of every speech, because, he once explained, “I am a sinner too.” His first tweet and first post on Instagram were versions of the mantra. – The poor – “How I…
- 21 Apr 2025 - The two have been warming up to each other with speculations on the future building up.
- 21 Apr 2025 - The Catholic faithful are set to get a new Pope after the death of Pope Francis on Easter Monday.
- 21 Apr 2025 - It is Easter. This is the period that Christianity worldwide commemorates the Passion of the Lord Jesus Christ, his crucifixion, and his triumphant rising from the dead. Jesus Christ was tried by Pontius Pilate, who was the prefect (governor) of Judea…
- 21 Apr 2025 - When a pope dies, the Roman Catholic Church begins a series of elaborate rituals.