- 387 viewsMajeshi ya Ukraine yameishambulia meli ya Russia iliyokuwa inawasili Crimea, shambulizi lililopiga sehemu ya meli kadhaa za Russia zilizoko katika bahari ya Black Sea ambazo jeshi la anga la Ukraine lilisema zinashukiwa kubeba droni zilizotengenezwa Iran. Wizara ya Ulinzi ya Russia ilisema kuwa shambulizi lililofanywa na Ukraine liliharibu meli ya Novocherkassk katika kituo cha Feodosia. Sergei Aksyonov, gavana wa Crimea aliyewekwa na Russia, alisema kupitia mtandao wa Telegram shambulizi hilo liliuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili. Mashirika ya habari ya Russia yaliripoti kuwa Rais Vladimir Putin alipewa muhtasari wa shambulizi hilo. Jeshi la anga la Ukraine lilisema limetumia makombora ya masafa marefu na kuwa shambulio hilo liliiteketeza meli hiyo. Kamanda wa jeshi la anga la Ukraine Mykola Oleshchuk alisambaza video kupitia mtandao wa Telegram ikionyesha mlipuko mkubwa huko Feodosia. “Na meli za Russia zinazidi kupungua zaidi,” Oleshchuk alisema. Jeshi la Ukraine pia limeripoti Jumanne kuangusha droni 13 kati ya 19 ambazo zilitumiwa na Russia kufanya mashambulizi usiku kucha. Lilisema droni hizo ziliangushwa huko katika mikoa ya Odesa, Kherson, Mykolaiv na Khmelnytskyi Russia ilidai Jumatatu kuwa majeshi yake yalikuwa yameteka mji wa kimkakati wa Maryinka ulioko mashariki mwa Ukraine, lakini Kyiv ilikanusha dai hilo, ikiripoti kuwa majeshi yake yalizima “mashambulizi matatu yaliyofeli” karibu na jamii ambayo imeharibiwa na kutelekezwa. “Si sahihi kuzungumzia kuiteka Maryinka,” msemaji wa jeshi la Ukraine Oleksandr Shtupun alikiambia kituo cha televisheni cha Ukraine kufuatia madai ya Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu wakati wa mkutano wake na Rais Vladimir Putin ulioonyeshwa kupitia televisheni. “Mapigano yanaendelea huko Maryinka,” Shtupun alisema. “Hivi sasa, wanajeshi wetu wako katika maeneo ya utawala ya mpakani huko Maryinka, lakini mji huo umeangamizwa kabisa,” alisema. Waliochangia katika ripoti hii ni Radio Free Europe/Radio Liberty Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Associated Press, Agence France-Presse and Reuters. #rais #vladimirputin #uhaini #wagner #usaliti #russia #joebiden #marekani #wagnergroup
Ukraine yaharibu meli kadhaa za Russia kwa makombora ya masafa marefu
- - Suagar Boy ››
- 30 Nov 2024 - The finance chief of India's Adani Group on Friday rejected U.S. allegations that executives, including Chairman Gautam Adani, were part of a Ksh.34 billion bribery scheme, while the Indian government said it has not received any U.S. request on the…
- 30 Nov 2024 - Disaster response teams coordinated by National Government Administration have begun evacuating over 240 households affected by the ongoing floods.
- 30 Nov 2024 - European and American carmakers are set to lose up to 17 per cent of their combined annual core profits if the U.S. imposes import tariffs on Europe, Mexico and Canada, S&P Global said in a report on Friday, warning of potential credit downgrades.
- 30 Nov 2024 - The Sambaza Furaha na Safaricom caravan was on Friday in its fifth day this week traversing the areas of Homa Bay, Rodi Kopany, Rongo, and Awendo.
- - Shame of Nakuru's dead not resting in peace: County fights claims of reuse of graves
- 29 Nov 2024 - Almost two months have lapsed since the Universal Health Coverage, through the Social Health Authority (SHA), was rolled out and the enrolment numbers into the programme are not yet up to the expected levels, with only 16 million registrations to date.
- 29 Nov 2024 - DCI officers spent the better part of Friday questioning some of the leaders and members of the public who attended the chaotic burial ceremony in Limuru, which saw goons attack former Deputy President Rigathi Gachagua and mourners.
- 29 Nov 2024 - The Jaramogi Oginga Odinga University of Science and Technology (JOOUST) will conduct an audit on all 2024 graduates before awarding any certificate amid reports of irregular awarding of degrees at the institution.
- 29 Nov 2024 - The Kenya Union of Clinical Officers (KUCO) has threatened to down their tolls beginning December 23, 2024 over what they term as discrimination in the rollout of the Social Health Insurance Fund (SHIF).
- 29 Nov 2024 - The Kenya Union of Clinical Officers (KUCO) has threatened to down their tolls beginning December 23, 2024 over what they term as discrimination in the rollout of the Social Health Insurance Fund (SHIF).