Upanzi wa miti Kwale

  • | Citizen TV
    262 views

    Kiwango cha misitu katika kaunti ya kwale kingali chini sana licha ya juhudi zilizowekwa za upanzi wa miti. Mhifadhi mkuu wa misitu eneo la Pwani James Mburu amesema Kwale ina asilimia 5.7 ya misitu ambayo iko chini ikilinganishwa na idadi inayolengwa ya asimilimia 30. Akizungumza kwenye zoezi la upandaji mikoko eneo la Mwazaro kaunti ya Kwale, Mburu amewataka wakaazi kuzidisha juhudi za ukuzaji wa miti hususan ile ya matunda ili pia kuongeza utoshelevu wa chakula.