Usaili wa mwenyekiti wa IEBC waingia siku ya pili

  • | KBC Video
    41 views

    Aliyekuwa naibu msajili mkuu wa idara ya mahakama Francis Kakai Kissinger ameliambia jopo linalowahoji watahiniwa wa nyadhifa mbalimbali katika tume ya IEBC kwamba alisimamishwa kazi na mahakama kwa kuidhinisha uchunguzi wa kesi ya sakata ya ufisadi ya shilingi milioni 300 mnamo mwaka 2015. Kissinger aliyekuwa miongoni mwa wawaniaji wanne waliohojiwa leo, alikanusha kuhusika na kesi hiyo ambapo ilipendekezwa afunguliwe mashtaka akiwa pamoja na aliyekuwa msajili mkuu wa idara ya mahakama wakati huo Gladys Boss Shollei kuhusiana na ununuzi wenye utata wa jumba la kifahari mtaani Runda la aliyekuwa jaji mkuu wakati huo. Abdiaziz Hashim ana maelezo ya kina kuhusu mahojiano hayo ya wadhifa wa uenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive