Video ya afisa wa KDF Abdullahi Issa anayezuiliwa na Al-Shabaab kwa miaka tisa

  • | K24 Video
    1,677 views

    Familia ya Abdullahi Issa Ibrahim anayedai kuwa mwanajeshi wa KDF imejitokeza kuzungumza baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Katika video hiyo Abdullahi anasema yeye alichukuliwa mateka tarehe 15 janujari mwaka wa 2016 wakati kundi la kigaidi la al shabab lilivamia kambi ya KDF El Adde nchini Somalia. mwanajeshi huyo mzaliwa wa kaunti ya ajir alikuwa akiishi eldoret. familia yake iliamini alifariki katika shambulio hilo na hata kuchukua cheti cha kifo miaka mitano baadaye.