Vijana Kisii waahidi mwamko mpya wa uongozi 2027

  • | Citizen TV
    1,491 views

    Saa chache baada ya aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kukiri kufanya mkutano na waziri wa zamani Dkt Fred Matiang'i, viongozi vijana kutoka kaunti mbalimbali mlima Kenya wameahidi mwamko mpya kwenye siasa za mwaka wa 2027. Wakizungumza katika makao makuu ya chama cha United Progressive Alliance mjini Kisii, vijana hao wamesema wakati umefika wa vijana kutumia idadi yao kwa madadiliko wa uongozi wa kitaifa