Vijana wakabiliana kwenye mazishi Matungu, Kakamega

  • | Citizen TV
    354 views

    Ghasia zilizuka kwenye mazishi ya aliyekuwa chifu katika kijiji cha matungu, eneo la Mumias kaunti ya Kakamega baada ya vijana walioandamana na wanasiasa kukabiliana na kuanza kupigana mazishini. Wafuasi wa gavana wa kakamega Fernandes Barasa na wa aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa walikabiliana kwenye mazishi hayo na kuilazimisha familia kukimbiza jeneza la marehemu kaburini.