Vijana wapinga mradi wa hewa ya kaboni Oldonyonyokie, Kajiado

  • | Citizen TV
    377 views

    Baadhi ya vijana kutoka eneo la Oldonyonyokie huko Magadi kaunti ya Kajiado wanapinga biashara ya hewa kaboni ambayo inaendeshwa na shirika moja katika eneo hilo, wakazi wakitarajiwa kutia saini mkataba na kampuni hiyo. Wakizungumza baada ya kuandaa mkutano katika eneo hilo, vijana hao wanasema wakazi hawafahamu vyema yaliyomo kwenye mkataba huo.