Vikundi 50 vyapewa mafunzo ya ujasiriamali wa plastiki Kwale

  • | Citizen TV
    71 views

    Vikundi 50 kutoka eneo la Shimoni na Vanga kaunti ya Kwale vimepokea mafunzo ya ujasiriamali kupitia ukusanyaji wa taka za plastiki. Mafunzo hayo yanalenga kukabiliana na utupaji wa kiholela wa plastiki kwa kuzizalisha ili kutengeza bidhaa zingine. Wanachama wa vikundi hivyo wameelimishwa jinsi ya kusimamia biashara zao na kutambua sera zilizopo katika sekta ya usimamizi wa taka.