Viongozi Baringo wataka wizi wa mifugo kutokomezwa baada ya chifu kuuawa na majambazi

  • | KBC Video
    20 views

    Viongozi katika kaunti ya Baringo wametoa wito wa kutokomezwa kwa wizi wa mifugo kwenye eneo hilo siku moja baada ya chifu mmoja kuuawa huko Chebilat katika eneobunge la Tiaty. Wakizungumza wakati wa hafla ya maombi ya madhehebu mbalimbali huko Chemolingot, hafla iliyohudhuriwa na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, viongozi hao walitaka kuwepo na amani kwenye maeneo yaliyopigwa na wimbi la wizi wa mifugo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive