Viongozi kadhaa kubuni mrengo mpya wa kisiasa

  • | KBC Video
    81 views

    Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha DAP-Kenya Eugene Wamalwa, kiongozi wa NARC Kenya Martha Karua, mwenzake wa chama cha PNU Peter Munya, Jeremiah Kioni wa chama cha Jubilee pamoja na aliyekuwa waziri wa usalama Dkt. Fred Matiangi, wamethibitisha kubuni muungano mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka-2027. Akiongea wakati wa uzinduzi wa makao makuu ya chama cha DAP-Kenya mtaani Karen, viongozi hao walithibitisha kubuniwa kwa mrengo wa kisiasa ambao walisema jina lake litafichuliwa hivi karibuni. Kiongozi wa DAP-Kenya Eugene na mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka, walisema muungano huo utachukua mahala pa ule wa Azimio.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive