Viongozi katika kaunti ya Homa Bay wahamasisha wasichana kujikinga dhidi ya mimba za utotoni

  • | Citizen TV
    263 views

    Viongozi wa kike katika kaunti ya Homa bay wameanzisha kampeni ya kuwahamasisha wasichana kuhusu mbinu za kujikinga dhidi ya mimba za utotoni haswa wakati huu ambapo wanafunzi wako likizoni. Viongozi hao na washikadau wengine wameeleza hofu yao kuhusu ongezeko ya idadi ya watoto wanaopachikwa mimba. Kaunti ya Homa Bay ni ya pili kitaifa kwa idadi ya wasichana wanaopata mimba wakiwa wachanga.