Viongozi kutoka Kaskazini Mashariki wasema eneo hilo limetengwa kimaendeleo

  • | Citizen TV
    318 views

    Viongozi kutoka kaskazini mwa nchi wameilaumu serikali kwa kile wanachodai kuachwa nje katika miradi ya maendeleo.Viongozi hao kutoka kaunti za Mandera, Wajir Na Garissa wanadai kuwa eneo hilo limetelekezwa kwa muda mrefu na sasa wanataka miradi ya kitaifa kufikishwa katika kaunti za kaskazini mwa Kenya ili kuimarisha biashara na maendeleo. Aidha wametaka jamii wa wafugaji Na maeneo kame nchini kuongzewa mgao wa pesa hasa katika miradi inayolenga kutatua uhaba wa maji Na utoshelevu wa chakula.