- 4,892 viewsDuration: 1:44Viongozi wa vuguvugu la Kenya Moja wameshtumu hotuba ya rais william ruto aliyowasilisha jana bungeni kitaifa wakisema ilijaa mambo yasiyo ya kweli na kusema kuwa rais alitumia bunge kuzindua manifesto yake ya mwaka 2027. Wakizungumza huko Magena, Bomachoge Borabu kaunti ya Kisii, katika hafla ya kupiga jeki vikundi vya wajane maeneo hayo, viongozi hao walipuuzilia mbali malengo ya Rais William Ruto ya ufanisi wa taifa wakisema hatilii maanani maswala muhimu kama vile kuboresha sekta ya Elimu, Afya na miundo msingi.