Viongozi wa kidini wameshtumu madai ya kunyanyaswa kwa waumini wa dhehebu la mashahidi wa Yehova

  • | KBC Video
    23 views

    Baadhi ya viongozi wa kidini wameshtumu madai ya kunyanyaswa kwa waumini wa dhehebu la mashahidi wa Yehova kwa misingi ya Imani yao nchini Eritrea wakitaja haua hiyo kuwa ukiukaji wa haki za kibinadamu. Kundi hilo limesema kuwa kuwabagua watu kwa misingi ya imani barani Afrika kunafaa kukomeshwa. Waumini wa dhehebu hilo humu nchini wamesema kuwa juhudi za kushinikiza kuachiliwa kwa wenzao wanaozuiliwa nchini Eritrea haijafauluWametoa wito kwa maafisa husika kuingilia kati suala hilo wakisema serikali ya Eretria iliwanyima mashahidi ya Yehova haki zao za kiraia na kisiasa mwaka 1994 baada yao kukaidi maagizo ya kushiriki katika uchaguzi na kuhuduma katika jeshi la nchi hiyo. Wanadai baadhi ya waumini hao wamekamatwa baada ya kuhudhuria mikutano ya kidini

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive