Viongozi wa kidini wataka siasa za uchaguzi kusitishwa

  • | Citizen TV
    43 views

    Viongozi wa Kidini kaunti ya Bungoma wamemkashfu Rais William Ruto kwa kuendeleza Kampeni ya Mapema miaka miwili kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2027. Viongozi hao wamemtaka rais kuwaongoza wale wanaoandamana naye kwenye kampeni hizo kuwajibikia majukumu yao badala ya kufanya siasa kila wakati. Aidha viongozi hao pia wametaja ushirikiano wa Rais William Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga kama unafiki.