Viongozi wa Murang'a wamtetea Ndindi Nyoro wakisema Nyoro alifanya maendeleo hata mbeleni

  • | Citizen TV
    1,263 views

    Viongozi na wakazi wa kaunti ya Muramg'a wamekosoa matamshi ya kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichingwa na mwenzake wa wachache Junet Mohammed kuhusu utendakazi wa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya bajeti bungeni Ndindi nyoro, ambaye pia ni mbunge wa kiharu. Viongozi hao wamemtetea Nyoro na kusema kuwa miradi ya ujenzi wa madarasa ya kisasa ilianza hata kabla ya yeye kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo. viongozi hao wamesema kuwa matamshi hayo ni njama ya kumharibia jina Ndindi Nyoro kutokana na misimamo yake ya kisiasa.