Viongozi wa Trans Nzoia wanapinga mswada wa kudhibiti makanisa

  • | Citizen TV
    166 views

    Viongozi katika Kaunti ya Trans Nzoia wanapinga mswada unaolenga kudhibiti makanisa wakisema kuwa mswada huo wa seneta danson mungatana una masharti yasiyofaa ,adhabu kali kwa mashirika ya kidini pamoja na mapendekezo ya kutoza kodi makanisa. Wakizungumza katika Shule ya Sekondari ya Botwa wakati wa hafla ya kukabidhi basi, viongozi hao walieleza wasiwasi wao, wakisema ni dhhaka kwamba wanasiasa, ambao mara kwa mara wanatafuta kura na baraka kutoka kwa makanisa wakati wa kampeni za uchaguzi, sasa wanapania kuanzisha sheria zinazowakandamiza. Pia walisisitiza msimamo wa Rais William Ruto kwamba viongozi wa kidini wana uwezo wa kudhibiti makanisa bila kuingiliwa kisiasa au na serikali.