Viongozi, Waumini wa Katoliki nchini watoa risala za rambirambi

  • | Citizen TV
    515 views

    Waumini wa kanisa Katoliki nchini wameungana na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Rais William Ruto na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kumwomboleza kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Francis. Viongozi wa kanisa hilo nchini wakiongozwa na askofu wa jimbo la Mombasa Martin Kivuva na askofu mwenza wa jimbo la Nyeri Anthony Muheria wamemtaja Papa Francis kama kiongozi aliyepigania watu wa tabaka la chini na usawa ulimwenguni kote.