Vipodozi vinaweza kuwa na madhara gani?

  • | BBC Swahili
    541 views
    Sasa hii ni kwa wale wanaojipodoa kama mimi... Lini mara ya mwisho ulikagua tarehe ya mwisho ya matumizi ya vipodozi vyako? Je, umewahi kufikiria kuwa vipodozi vilivyoisha muda wake vinaweza kuharibu ngozi yako, au hata kuhatarisha afya yako? Au je, umewahi kuazima brashi ya kupakia kipodozi kutoka kwa rafiki au kujipaka rangi ya mdomo dukani? Wanasayansi waligundua bakteria wabaya kwenye sampuli za vipodozi zilizopitwa na muda, kama vile bakteria aina ya Candida Yeast na E Coli.