Visa vya moto vimeshuhudiwa katika mbunga kadhaa nchini

  • | Citizen TV
    1,727 views

    Visa vya moto vimeshudhuiwa katika mbunga kadhaa za wanyamapori na misitu humu nchini kutokana na shughuli za binadamu na kiwango cha juu cha joto kinachoshuhudiwa nchini. Idara ya huduma kwa wanyamapori - KWS- Imewaonya wananchi dhidi ya kuwasha mioto kiholela au kutupa vipande vya sigara wakati huu ambapo kuna ukavu. Na kama anavyoarifu Emily Chebet, mbuga ya wanyamapori ya Nairobi ndio ya hivi punde kushuhudia moto.