Vituo vya afya vya kidini vyaitaka serikali kulipa madeni ya NHIF ndani ya siku 14

  • | K24 Video
    53 views

    Vituo vya afya vya kidini nchini vimeipa serikali siku 14 kulipa madeni ya nhif na kukamilisha malipo ya huduma zinzotolewa chini ya mamlaka ya afya ya jamii,SHA. Iwapo serikali haitatimiza hilo,huduma chini ya sha zitasitishwa katika vituo hivyo. Taasisi hizo zinasema zimelemewa kifedha kutokana na madeni ambayo bado hayajalipwa.wakati huo huo, chama cha hospitali za kibinafsi za miji na vijijini (RUPHA) kimeondoa marufuku ya huduma za sha katika hospitali zake. Hatua hii inafuatia ahadi ya Rais William Ruto ya kulipa madeni yote ya nhif chini ya shilingi milioni kumi .