Waandamanaji wabeba bendera za Russia wakilalamikia hali ngumu ya uchumi

  • | VOA Swahili
    870 views
    Mkuu wa Wafanyakazi wa Jeshi la Ulinzi Nigeria, Jenerali Christopher Musa, ameeleza kupeperusha bendera ya kigeni wakati wa maandamano dhidi ya serikali ni “kosa la uhaini” baada ya kufanya mazungumzo na Rais Bola Tinubu Jumatatu. Maelfu ya watu wamejitokeza mitaani huko Kano, mji mkuu Abuja, na miji mingine mikubwa wakati wa maandamano dhidi ya hali ngumu ya uchumi na uhalifu. Shirika la Amnesty International lilisema kuwa watu wasiopungua 13 wameuwawa katika mapambano na polisi tangu kuanza kwa maandamano hayo, ambayo yamepewa jina “#10DaysOfRage.” Polisi wameeleza idadi ya vifo ni saba, wakisema baadhi ya vifo vilitokana na ajali mbalimbali na vilipuzi. (Reuters) #nigeria #russia #tinubu #voa