Waandamanaji walaani mauaji yanayoendelea Gaza mbele ya Ubalozi wa Israel Amman

  • | VOA Swahili
    179 views
    Waandamanaji walikusanyika karibu na ubalozi wa Israel huko Amman, Jordan leo Ijumaa kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza. Takriban watu 250 walionekana kwenye maandamano hayo, wakibeba mabango na kuimba nyimbo. Katika siku za hivi karibuni, Israel imetoa amri kadhaa zaidi za wakazi wa Gaza kuondoka tangu kuanza kwa vita vya miezi 10, na kusababisha malalamiko kutoka kwa Wapalestina, Umoja wa Mataifa na maafisa wa misaada juu ya kusitishwa kwa misaada ya biandamu kufikia maeneo ya kibinadamu na kutokuwepo kwa maeneo salama. Shambulizi la hivi punde katika mzozo wa miongo kadhaa kati ya Israel na Palestina ulichochewa Oktoba 7 wakati kundi la Palestina la Hamas liliposhambulia Israel, na kuua 1,200 na kuchukua mateka wapatao 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israel. Mashambulio yaliyofuata ya Israel dhidi ya eneo linalotawaliwa na Hamas tangu wakati huo yameua zaidi ya Wapalestina 40,000, kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo hilo, huku pia ikiwafukuza karibu watu wote milioni 2.3, na kusababisha baa la njaa na kusababisha madai ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Dunia ambayo Israel inakanusha. - Reuters ⁣ #gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina ⁣