Waandishi wakabiliana na habari potofu kuhusu chanjo kuondoa kizazi na athari kwa jamii

  • | VOA Swahili
    8 views
    Katika eneo linalopambana na changamoto za afya na kukumbwa na vita, waandishi wa kubaini habari za uongo katika jarida la Eleza ukweli mjini Goma, DRC, wanatafuta habari za ukweli kuhusu fikra zinazoambatana na ugonjwa mpox ambao awali ulikuwa unajulikana kama ugonjwa kutoka kwa nyani. Habari za uongo zinasema kwamba ugonjwa huo haupo kabisa na kwamba yanayosemwa ni upele tu ambao hauna madhara. Aline Kataliko anasema kazi yao ni muhimu sana kwa afya ya umma na katika kujenga imani katika jamii. Aline Kataliko wa Eleza Fact: 'Kuna uvumi kuhusu mpox, unaosema kwamba lengo la chanjo ni kuondoa kizazi cha raia wa Congo. Tunaangazia hatari za uvumi huo na namna unavyoweza kuathiri jamii yote kwa jumla na kuzuia juhudi za kumaliza maambukizi." Tangu mwaka 2021, waandishi wa habari 25 katika jarida la Eleza ukweli, akiwemo Joel Alimasi Kitambala, wamekuwa wakiangazia na kueneza habari kuhusu hatari za habari potofu. Joel Alimasi Kitambala ni mwandishi wa habari katika Eleza Ukweli. Joel Alimasi Kitambala wa Eleza Fact: Kutambua ukweli, tunatumia maneno muhimu na kila wakati kuna chapisho ambalo lina maneno hayo, tunapata taarifa kuhusu chapisho hilo. Kama kuna hja ya kuchambua jarida hilo, waandishi wa kutafuta ukweli wanapewa jukumu wanaolifanyia kazi. Makala yanayochapishwa na Eleza ukweli, yanachapishwa kwenye wavuti, na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kutangazwa kwenye vituo vya radio ili kuwafikia wale wasiotumia internet. #habaripotofu #drc #goma #waandishi #voa #voaswahili