Wabunge wanasema uamuzi wa kubatilishwa kwa mikataba ya Adani utaokoa pesa za umma

  • | Citizen TV
    766 views

    Wabunge wengi wamepongeza uamuzi wa Rais William Ruto kuagiza kubatilishwa kwa mkataba kati ya serikali na kampuni ya India ya Adani. Wakizungumza pindi baada ya hotuba ya Rais katika majengo ya bunge, wengi wamesifia uamuzi huu wanaosema utaokoa mali ya umma. Hata hivyo, baadhi wana wasiwasi kuhusu gharama za kubatilishwa kwa mkataba kati ya kampuni ya kusambaza umeme ya KETRACO na Adani.