Wadau Homa Bay wabuni chama kutetea maslahi ya waathiriwa wa kisukari

  • | KBC Video
    1 views

    Kundi moja la wagonjwa wa kisukari katika kaunti ya Homabay limebuni chama kwa lengo la kushinikiza huduma bora za matibabu na kushughulikia changamoto zinazowasibu waathiriwa. wakiongea katika shule moja ya msingi katika kaunti ya Homa Bay wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya ugonjwa wa kisukukari wanachama wa kundi hilo wakiongozwa na Mboya Thomas Joseph walielezea kujitolea kwao katika kuboresha huduma za matibabu ya wagonjwa wa kisukari .Mshirikishi wa shirika la matabibu wasiokuwa na mipaka katika kaunti hiyo Dr. Bright Mukhuna aliwahimiza wakazi kufanyiwa uchunguzi wa kila mara ili kubaini mapema iwapo wanaugua kisukari na kupata tiba kwa wakati ufaao

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive