Wadau katika sekta ya madini Taita watoa lalama zao

  • | K24 Video
    41 views

    Huku sekta ya madini humu nchini ikiendelea kuvutia wengi, wadau katika sekta hiyo hasa ukanda wa pwani wamepinga mpango wa serikali kuu wa kuorodhesha madini aina ya tsavorite kama moja wapo wa madini muhimu ya kimkakati humu nchini. Wamesema mpango huo huenda ukaua kabisa sekta ya madini hasa katika maeneo ya mkuki, kabanga na kamtonga yalioko mwatate sawia na maeneo ya kaunti ya kwale yanayotoa madini sampuli hiyo kwa wingi. mwanahabari wetu joel mburia ana mengi kutoka Voi.