Wafanyabiashara walalamikia hali ya soko la Katito huko Kisumu

  • | Citizen TV
    356 views

    Wafanyabiashara katika soko la Katito wanaitaka serikali ya kaunti ya Kisumu kuzoa taka katika soko hilo ili kuwaepushia mlipuko wa magonjwa. Akizungumza sokoni humo, mwenyekiti wa wafanyabiashara katika soko hilo Abdala Otieno amesema kuwa mabomba ya maji yamezibwa na takataka na kusababisha mafuriko katika soko hilo.