Wafanyibiashara Nanyuki watoa mafunzo kwa familia zinazoishi mitaani

  • | Citizen TV
    259 views

    Katika juhudi za kupunguza idadi ya watoto wanaorandaranda mjini Nanyuki wanabiashara mjini humo wameanzisha shule ya kiufundi itakayowapa wanarika na watoto kutoka kwenye familia zisizojiweza masomo ya kuwawezesha kujikimu kimaisha. Baadhi ya taaluma hizi ni uokaji wa mikate na keki,ususi na muziki. biashara hizo zinalenga kuwapa fedha za kulipia karo. Msimamizi wa shule hiyo Paul Mwaniki amewarai Wakenya kuanzisha miradi kama hiyo ili kuwapa vijana ujuzi utakaowawezesha kujitegemea na kuendeleza maisha Yao.Kwa miaka 2 Sasa, shule hiyo imewasaidia wanafunzi 300 kupata ujuzi. Shule hiyo inalenga kuwafunza wanafunzi 10,000 kufikia mwaka wa 2027.