Wafugaji wa mpaka wa Narok - Nakuru wahimiza amani

  • | Citizen TV
    187 views

    Wafugaji wanaoishi kwenye mpaka wa Kaunti za Narok na Nakuru wamehimizwa kuishi kwa amani na kutatua mizozo ya kila mara kupitia asasi za serikali na wazee wa mitaa. Akizungumza baada ya uzinduzi rasmi wa mnada wa Ole Tipis katika kituo cha biashara cha Mwisho-lami Narok Kaskazini, Kamishna wa Narok Kipkech Lotiatia, alisema kuwa mkutano mkubwa umeandaliwa ili kuwahamasisha wakazi kuhusu umihimu wa amani. Gavana wa Kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amesema kuwa malisho ya mifugo na maji imesababisha migogoro ya mara kwa mara.