Wagonjwa wanaotegemea matibabu ya ARVs wakumbwa na uhaba wa dawa hizo Kisumu

  • | K24 Video
    7 views

    Imepita miaka 41 tangu kisa cha kwanza cha virusi vya HIV kuripotiwa nchini Kenya, na taifa limepiga hatua kubwa katika kudhibiti janga hilo. Hata hivyo, changamoto mpya sasa inahatarisha mafanikio hayo. Wagonjwa wanaotegemea matibabu ya kiwango cha pili cha dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs) wanakumbwa na uhaba wa dawa muhimu kufuatia kuhamishwa kwa kiwango cha kwanza kutoka kwa cha pili.