Wahadhiri kugoma tena

  • | Citizen TV
    1,574 views

    Wanafunzi wa vyuo vikuu wakijiandaa kurejelea masomo wiki ijayo, huenda wakalazimika tena kurejea nyumbani baada ya majuma mawili. Hii ni baada ya muungano wa wahadhiri nchini -uasu- kutoa makataa ya siku kumi na tano kuanzia leo Januari mosi kwa serikali kulipa mshahara wa Disemba pamoja na malimbikizi yote waliyofaa kupokea tangu Septemba. Wahadhiri wanateta kuwa serikali imepuuza makubaliano kuhusu nyongeza ya mshahara.